NACTE : TAARIFA KWA UMMA – KUHUSU KUHAMA KWA OFISI YA NACTE KANDA YA KASKAZINI

By | August 3, 2017

NACTE : TAARIFA KWA UMMA – KUHUSU KUHAMA KWA OFISI YA NACTE KANDA YA KASKAZINI

TAARIFA KWA UMMA
 
KUHUSU KUHAMA KWA OFISI YA NACTE KANDA YA KASKAZINI
 
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), linapenda kuuhabarisha Umma na wadau wa Elimu nchini hasa wa kanda ya Kaskazini ya kwamba, ofisi ya baraza ya kanda ya kaskazini imehamia katika jengo jipya la NSSF COMMERCIAL COMPLEX (MAFAO HOUSE) ghorofa ya nane (8), jengo hili lipo katika barabara ya Old Moshi, Plot No. 1. Karibu na New Arusha Hotel kuelekea Kibo Palace Hotel.
 
Kabla ya kuhama ofisi hizo zilikuwa katika majengo ya Arusha Technical College (ATC) Chumba namba nne (4), karibu na njia panda ya barabara ya kuelekea Nairobi (Namanga Road) na ile inayotoka Moshi.
 
Kwa maelezo zaidi, wasiliana na Ofisi zetu za Kanda ya Kaskazini kwa anuani zifuatazo;-
 
NACTE Northern Zone
P.o. Box 14333 Arusha,
Mobile: 0658444556/57
Email: northern.zone@nacte.go.tz
 
 
IMETOLEWA NA;
KITENGO CHA HABARI MAWASILIANO
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
3/08/2017
See also

National Council for Technical Education | NACTE |

Admissions for Universities in Tanzania

Examination Results for Universities in Tanzania

Selected Candidates / Applicants

Necta Examination Results

International Scholarships for Tanzanians to Study Abroad